ofisi ya rais ikulu
play

OFISI YA RAIS, IKULU M PANGO WA UENDESHAJ I WA SHUGHULI ZA - PowerPoint PPT Presentation

OFISI YA RAIS, IKULU M PANGO WA UENDESHAJ I WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERM ENT PARTNERSHIP OGP) Imewasilishwa kwenye M kutano wa M ashauriano na Wadau 15 Novemba 2011 1 Yaliyomo Utangulizi Chimbuko la M pango


  1. OFISI YA RAIS, IKULU M PANGO WA UENDESHAJ I WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERM ENT PARTNERSHIP – OGP) Imewasilishwa kwenye M kutano wa M ashauriano na Wadau 15 Novemba 2011 1

  2. Yaliyomo • Utangulizi • Chimbuko la M pango • M aeneo yanayozingatiwa kwenye M pango • M aandalizi ya M pango wa Tanzania • Ni maeneo yapi yaingizwe kwenye M pango wa Kitaifa? • M anufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekeleza OGP • Hitimisho 2

  3. Utangulizi • Tangu tupate Uhuru mwaka 1961 juhudi zimekuwa zikifanywa na Serikali katika Awamu zote za kuhakikisha wananchi wanahusishwa na kupewa habari kuhusu mustakabali wa maisha yao. • Katiba ya Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Ibara za 18(d), 20(1), na 21(2) zinazungumzia ushiriki wa Wananchi katika kupata habari na kushiriki katika shughuli zinazohusu maendeleo yao. • Ili kutimiza matakwa haya ya Kikatiba Serikali ilibuni M wongozo wa Utawala Bora unaozingatia misingi ya demokrasia, uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji, usawa, utawala wa sheria, na uadilifu. 3

  4. Utangulizi (unaendelea) • Serikali imeandaa Sera mbalimbali ili kuhakikisha misingi ya Utawala Bora inazingatiwa. Baadhi ya Sera hizo ni kama vile Sera ya Afya ya mwaka 2007, Sera ya Elimu na M afunzo ya mwaka 1995, Sera ya M aji ya mwaka 2002 zinatamka wazi kwamba ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu. • Utekelezaji wa M pango huu siyo jambo geni machoni mwa Watanzania. Lengo la mpango huu ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utendaji wa shughuli za Serikali. 4

  5. Chimbuko la M pango • M pango huu wa uendeshaji Serikali kwa uwazi (OGP) ulibuniwa na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali, M ashirika yasiyo ya Kiserikali na kuzinduliwa M jini New Y ork M arekani tarehe 20 Septemba 2010. • Serikali ya Tanzania imeridhia kujiunga katika M pango huu unaojumuisha Nchi nyingine 45 duniani ambapo Nchi kutoka Afrika ni Kenya, Ghana, Liberia na Afrika ya Kusini. 5

  6. Chimbuko la M pango - unaendelea Chimbuko la mpango huu linatokana na changamoto nyingi kuendelea kujitokeza katika uendeshaji wa shughuli za Serikali zetu kama vile • Kuimarisha uadilifu miongoni mwa Watumishi wa Umma, • M atumizi mazuri ya rasilimali za Nchi, • Kuimarisha usalama wa wananchi • Uwajibikaji wa kitaasisi 6

  7. Chimbuko (linaendelea) M pango unajikita katika maeneo makuu manne:- – Uwazi – Ushirikishwaji wa wananchi – Uwajibikaji – Teknolojia na Uvumbuzi Equity M onitoring Report, 2011 7

  8. Chimbuko la M pango - inaendelea • M atokeo yanayotarajiwa yako katika maeneo makuu matano: – Kuboreka kwa utoaji wa huduma – Kuongezeka kwa uadilifu – Kusimamia ipasavyo matumizi ya mali za umma – Kuongeza usalama wa wananchi – Kuongezeka kwa uwajibikaji wa Kitaasisi. 8

  9. Taratibu za Nchi Kujiunga na OGP • Nchi zilizojiunga zinasaini makubaliano ya kujiunga • Baada ya kusaini zinaainisha maeneo kwa kushirikiana na wadau ambayo zinadhani yataimarisha uwajibikaji na kutayarisha mpango Kazi • M pango utakaotayarishwa unawasilishwa kwenye Sekretarieti ya Kimataifa kwa ajili ya kupata uzoefu wa Nchi zingine shiriki kwenye M pango • Utekelezaji pamoja na tathmini unafanyika 9

  10. Hatua zilizofikiwa kwa Tanzania • Kikundi Kazi kimeundwa na Serikali kusimamia uandaaji wa M pango wa Kitaifa wa OGP • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora,tayari ametoa taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuhusu mkakati wa kutayarisha M pango huu • M aelekezo yametolewa kwa kila Wizara kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika M pango huu wa ‘OGP’ • TWAWEZA ni mdau muhimu katika maandalizi ya M pango huu. 10

  11. Hatua zilizofikiwa kwa Tanzania • Ili kuweza kujipima kikamilifu, Tanzania imeamua kuanza kutekeleza mpango huu katika Sekta tatu za huduma za jamii ambazo ni Afya, Elimu, na M aji • Ili kushirikisha wananchi wengi zaidi katika kutoa maoni namba ya Wazi na bure ya simu imetolewa kwa wananchi kupiga simu au kutuma ujumbe (sms) bila malipo. Namba hiyo ni 0658 - 999222 • Kutoa anwani kwa wananchi wanaotaka kutumia njia ya barua: IKULU, SL.P . 9120 DAR ES SALAAM . • Kutoa anwani za tovuti: www.mwananchi.go.tz 11

  12. Ni maeneo yapi yaingizwe kwenye M pango wa Kitaifa? • Uwazi: – Kuweka utaratibu wa kuyafanya madawati ya malalamiko yaliyoanzishwa katika Wizara na M amlaka za Serikali za M itaa yafanye kazi. Hii itaongeza uwazi katika utendaji wa shughuli za Serikali – Kubaini na kuimarisha matumizi ya masanduku ya maoni yaliyopo katika vituo vya kutolea huduma na kuweka utaratibu madhubuti wa kutambua yanavyofanya kazi 12

  13. • Uwazi (inaendelea): – Kupitia upya majukumu ya Bodi na Kamati za Vituo vya utoaji wa huduma katika Sekta za Afya, Elimu na M aji ili kuzifanya zitekeleze majukumu yake ipasavyo – Kuweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa taarifa za mapato na matumizi zinabandikwa katika M bao za M atangazo kwenye ngazi za Halmashauri, Kata, Vijiji, M itaa na Vituo vya kutolea huduma katika Sekta za Afya, Elimu na M aji 13

  14. • Ushirikishwaji: – Kuweka taratibu madhubuti na rahisi za kufanya tovuti ya Wananchi iweze kutumika kikamilifu. – Kupitia upya mfumo wa Upangaji wa M ipango ngazi za M singi kwa kutumia utaratibu wa fursa na vikwazo (O&OD) ili uwe rahisi kutumika na wananchi na kuleta matokeo tarajiwa. – Kupitia upya miongozo na taratibu za uendeshaji mikutano ya M ashauriano na Wadau juu ya Upangaji M ipango na Bajeti katika Sekta za Afya, Elimu na M aji kwa lengo la kupata ushiriki mpana zaidi na hivyo kuongeza ushirikishwaji. 14

  15. • Uwajibikaji na Uadilifu: – Kuhuisha M ikataba ya huduma kwa M teja katika Wizara na M amlaka za Serikali za M itaa ili kuhakikisha yaliyomo yanatekelezwa – Kuimarisha taratibu zilizopo za ufuatiliaji wa M apato na M atumizi ya fedha za Umma (Public Exependiture Tracking Survey – PETS) kwa lengo la kubaini thamani ya fedha. – Kuhuisha vigezo vya utoaji wa ruzuku ya matumizi ya Kawaida na M aendeleo katika Halmashauri. – Kuweka taratibu madhubuti za kusimamia mapato na matumizi ya fedha kwa kutumia ‘Integrated Financial M anagement System’ (IFM S), ambayo imewekwa katika M ikoa, Wizara na Halmashauri zote 15

  16. • Teknolojia na Uvumbuzi: • Kuandaa ramani zinazoainisha vituo/ maeneo ya utoaji wa huduma za maji Nchini ili taarifa hizo zitumike kupanga mipango endelevu ya maji. Utaratibu huu utasaidia wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wao kuhusu ufanyaji kazi wa vituo vya maji vilivyopo. • Kuongeza kasi ya matumizi ya TEHAM A katika kuongeza ufanisi wa kufundishia na kujifunzia. • Kuhakikisha teknolojia ya matibabu kwa njia ya masafa (telemedicine) inatekelezwa kama ilivyotarajiwa. M pango huu ambao umeanzia ‘Ocean Road Hospital’ utaenezwa katika Hospitali nyingine nchini. • Kutoa taarifa mbalimbali za utoaji wa huduma (Elimu, Afya, M aji) kwa wananchi kwa kutumia njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama vile tovuti, simu za mkononi, televisheni, kompyuta, radio na sms. OGP Taskforce, Tanzania 16

  17. M anufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekeleza OGP Uzoefu unaonyesha kwamba Nchi ambazo zimeanza kutekeleza M pango wa OGP zimepata mafanikio makubwa katika kuboresha utoaji huduma na kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Baadhi ya Nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia M pango huu ni: • M exico – Kupitia CSO ijulikanayo kama FUNDAR ilionyesha upungufu wa utoaji huduma kwa akina mama ambapo Zahanaji zilikuwa hazifunguliwi na haduma za dawa hazipatikani. Kwa kutumia matangazo ya CSO hii Wizara ya Afya ilishughulikia tatizo hili na kuokoa maisha ya watu. Equity M onitoring Report, 2011 17

  18. M anufaa yaliyopatika kwa Nchi zilizoanza kutekeleza OGP (Yanaendelea) • India – M KSS walihamasisha ubandikaji wa taarifa mbalimbali zipatazo laki moja kwenye mbao za matangazo zilizosaidia wananchi kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Jimbo la Rajasthan Equity M onitoring Report, 2011 18

  19. HITIM ISHO • M pango huu wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi utasaidia Taifa letu kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika kuchangia mawazo, maoni, na mapendekezo juu ya uendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali. Hatua hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma kulingana na vipaumbele vilivyowekwa na hivyo kuharakisha maendeleo. Ni vema nafasi hii ikachukuliwa kwa uzito wake na wadau wote. • Asasi za Kiraia (CSOs) zina jukumu la msingi na la kipekee katika kufanikisha hili. Tushirikiane wote kuendeleza kasi ya maendeleo ya Taifa letu. • Kwa taarifa zaidi kuhusiana na OGP tafadhali tembelea: www.opengovpartnership.org OGP Tanzania 19

Download Presentation
Download Policy: The content available on the website is offered to you 'AS IS' for your personal information and use only. It cannot be commercialized, licensed, or distributed on other websites without prior consent from the author. To download a presentation, simply click this link. If you encounter any difficulties during the download process, it's possible that the publisher has removed the file from their server.

Recommend


More recommend